BOCCO AICHIMBA MKWARA YANGA FAINALI SHIRIKISHO

 


MSHAMBULIAJI na nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco ameweka wazi kuwa, kikosi chao kimejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili ijayo.

Simba na Yanga zitakutana Jumapili ijayo ya Julai 25, katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho utakaochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara wataingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga Julai 3, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Bocco amekuwa katika kiwango bora msimu huu, ambapo amefanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 16.

Akizungumzia mchezo huo wa fainali Bocco amesema: “Tunatarajia kukutana na mchezo mgumu wa fainali dhidi ya Yanga, hii ni kwa sababu wapinzani wetu wana timu nzuri na tunawaheshimu kwa hilo.

“Lakini nasi tuna timu nzuri sana, hivyo tunakwenda kufanya maandalizi yaliyokuwa bora, na tunaamini katika maandalizi yetu kuwa tunakwenda kushinda mchezo huo.”

Post a Comment

0 Comments