Home Simba SC HANS POPE – MANARA KAPEWA MILIONI 10 NA GSM

HANS POPE – MANARA KAPEWA MILIONI 10 NA GSM


MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hanspope, amesema kitendo cha msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara kusambaza sauti ikimtuhumu CEO, Barbara Gonzalez wa timu kuelekea mchezo wa Kombe la TFF ni kuihujumu timu.

Hanspope amefunguka hayo kama mwanachama na sio kiongozi wa timu hiyo huku akiweka wazi kuwa Simba ni timu kubwa haiwezi kumjubu.

Amesema Manara hakuwa na sababu ya kuzungumza mambo ya ndani mitandaoni alikuwa na nafasi ya kumtafuta kiongozi huyo au kwenda ngazi ya juu ili wayamalize kwa alichokifanya anakichukulia kama ni kuhujumu timu kuelekea mchezo wa ‘dabi’ unaotarajiwa kuchezwa Jumapili.

“Amekosa maadili kama hakuridhika na alichofanyiwa na CEO na yeye ni binadamu kama wengine anaweza kuwa anakosea lakini sio kwa namna aliyoitumia angeweza kwenda ngazi za juu apeleke malalamiko kwenye bodi,” amesema.

“Tukianza kuunganisha matukio tunaweza kusema anatumwa na hao watu anaowafanyia kazi maana mtu anapelekwa kwenye michango ya harusi analipwa Sh10 millioni eti michango ya harusi kumbe ni hongo kwa kazi fulani tunajua haya mambo yanatoke,” amesema Hanspope ambaye ameweka wazi kuwa yupo Simba kwaajili ya kuitengeneza timu hiyo iwe imara.

SOMA NA HII  SIMBA: TUTAPATA PENALTI 5 MBELE YA YANGA