JEMBE JIPYA AZAM LACHIMBA MKWARA MZITO


BEKI mpya wa kushoto wa klabu ya Azam, Edward Charles Manyama amefunguka kuwa amejipanga kuhakikisha anapambana kwa ajili ya kuhakikisha anakuwa sehemu ya mafanikio ya waajiri wake hao wapya.

Manyama tayari ametangazwa rasmi kujiunga Azam akitokea ndani ya kikosi cha klabu ya Ruvu Shooting aliyohudumu kwa muda mfupi, kutokea ndani ya kikosi cha Namungo.

Akizungumza baada ya kukamilisha usajili wake ndani ya Azam, Manyama amesema: "Nimefurahi kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na klabu ya Azam, kwangu kujiunga na klabu hii ilikuwa ni ndoto yangu.

“Nimejipanga kuhakikisha najitolea, nitajituma kadiri ya uwezo wangu ili klabu yetu iweze kuendelea mbele."

Post a Comment

0 Comments