KOCHA AIPA TANO YANGA KUINASA SAINI YA MAYELE


BAADA ya Yanga kukamilisha usajili wa mshambulaiji wa AS Vita, Fiston Mayele, kocha msaidizi wa AS Vita Roul Shungu amesema kuwa Yanga imefanikiwa kumpata mshambuliaji mzuri atayekwenda kuwasaidia kufunga mabao ya kutosha katika safu ya ushambuliaji msimu ujao.


Shungu aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga 
kuanzia mwaka 1998- 2001 na kufanikiwa kuipatia ubingwa wa ligi kuu katika msimu wa mwaka 1999/2000.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka DR Congo, Shungu alisema kuwa Fiston Mayele ni moja kati ya washambuliaji bora wanaopatikana kwa sasa nchini Congo huku akisema kuwa njaa yake ya kufunga imekuwa ikimsaidia kufanya vizuri jambo ambalo anaamini pia atalifanya na kwa Yanga pia.

“Mayele ni mshambualiaji mzuri sana, kwa hapa Congo ni moja kati ya washambuliaji bora,utaona hata katika michuano ya CHAN yeye ndiye alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya DR Congo na hata katika Klabu ya AS Vita yeye ndiye kinara wa kufunga katika msimu uliopita ndani ya timu.

 

“Hivyo hata Yanga huko anapokwenda naamini atafanya vizuri sana kwa kuwa ni mchezaji anayejua kufunga na ana njaa ya kufunga, kwetu sisi tunamtakia kila la kheri huko anapoenda na huo ndio maana ya mpira,” alisema kocha huyo.Post a Comment

1 Comments