MAJEMBE MATATU YA KAZI YANGA KUANZA KAZI


 UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa tayari wachezaji wake wote watatu ambao walikuwa na matatizo ya kinidhamu wamekubali makosa yao na kuomba msamaha hivyo watarejeshwa kwenye mazoezi.

Nyota hao ni pamoja na beki Lamine Moro, mshambuliaji Michael Sarpong ambao wote kwa pamoja wametupia mabao manne ndani ya ligi kwa kila mmoja.

Ni Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi aliwatimua kutokana na makosa yao ambapo tayari kwa sasa raia hao wa Ghana wamerejeshwa kikosini.

Kwa upande wa nyota mwingine ni mzawa, Metacha Mnata ambaye alionyesha ishara za matusi kwa mashabiki wake baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Ruvu Shooting v Yanga.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wachezaji hao wamerejeshwa kikosini baada ya kukiri kufanya utovu wa nidhamu.


"Moro na Sarpong wataingia rasmi kambini baada ya mchezo wetu dhidi ya Ihefu ambao ni wa ligi hivyo wataanza kuwa pamoja nasi kwenye maandalizi ya kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho tutakaocheza dhidi ya Simba," .

Pia Mnata tayari amerejeshwa kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo kwa kuwa alikuwa amesimamishwa kwa muda usiojulikana. Post a Comment

0 Comments