Home news HAJI MANARA: SENZO ALIAJIRIWA ILI ANIFUKUZE

HAJI MANARA: SENZO ALIAJIRIWA ILI ANIFUKUZE

 HAJI Manara aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba,  Senzo Mbatha aliajiliwa ili aweze kumfukuza kazi.

Haji alibwaga manyanga ndani ya Simba kupitia kundi la Simba HQ baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na mabosi wa Simba.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Manara amesema kuwa alipoletwa Mbatha kutoka Afrika Kusini aliniita ofisini na kuniambia kwamba waajiri wamemuambia kazi yake ya kwanza ni kumfukiza yeye.

“Senzo aliniita ofisini akaniambia kwamba kazi ya kwanza ambayo amepewa na mabosi waliomuajiri ni kumfukuza kazi yeye jambo ambalo yeye alilikataa.

Mbatha aliniambia kwamba hakuona maana ya kunifukuza kwa kuwa alikuwa hajafanya nami kazi na aliona ile Simba day ya 2019 hivyo ni mtu muhimu. 

“Nilibaki Simba ila kwa kuwa ilikuwa hivyo nikafanya naye kazi kwa ushirikiano na kila kitu kiliendelea mpaka pale ambapo Senzo akaondoka nikajua kwamba anayefuata ni mimi,” amesema Haji Manara.

SOMA NA HII  TIZI LA YANGA SIO POA KAMA ULAYA UNAAMBIWA