Home kimataifa ADAM TRAORE, MWILI JUMBA MATAJI MATATU

ADAM TRAORE, MWILI JUMBA MATAJI MATATU


MWILI jumba unambeba huyu jamaa ambaye aliletwa duniani Januari 25,1996 ana umri wa miaka 25 ni raia wa Hispania huyu mwamba ambaye anakipiga ndani ya Wolves.

Licha ya wengi kumjadili kuhusu mwili wake huku akiweka wazi kuwa ni mazoezi pamoja na msosi ila amenyanyua mataji matatu kwa sasa na sio ndani ya Ligi Kuu England bali alikuwa Hispania huko.


Alijiunga na Wolves inayoshiriki Ligi Kuu England, Agosti 8,2018 na mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 30,2023 hivyo kwa sasa bado yupoyupo na timu ambayo inasaka saini yake lazima ijipange kuvunja mkataba wake.

Akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania kwenye mashindano ya Euro 2020 rekodi zinaonyesha kuwa alicheza mchezo mmoja hakuweza kuonyeshwa kadi ya njano hata nyekundu pia licha ya kuaminika kutumia mabavu mengi awapo uwanjani.

Ni Winga ambaye amenyanyua mataji matatu katika maisha yake ya soka kwa wakati huu na bado anaendelea kupambana kwa kuwa umri unamruhusu kufanya hayo yote.

Moja ya taji ambalo alitwaa ni lile la La Liga akiwa na Barcelona msimu wa 2014/15, Spanish Super Cup msimu wa 2013/14 na UEFA U 19 akiwa na Barcelona msimu wa 2013/14.

Mbali na Barcelona pia alicheza ndani ya Aston Villa msimu wa 2015/16 na alicheza jumla ya mechi 11 pia alicheza Middlesbrough mechi 61 na alitupia mabao 5.

SOMA NA HII  ARSENAL YAMPIGIA HESABU LAUTARO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here