BAADA YA KUIONA SIMBA VS MAZEMBE JUZI..SHABAN DJUMA AGUNA KISHA ATOA KAULI KUELEKEA GAME YA KESHO KUTWA


YANGA na Simba ziliingia kambini jana jioni tayari kwa vita ya dakika 90 pale Uwanja wa Mkapa Jumamosi.

Lakini ‘beki mshambuliaji’ wa Yanga, Djuma Shabaan amedai liwalo na liwe Jumamosi kwenye lazima washinde ngao ya jamii kulinda heshima yao.

Djuma ambaye amezikosa dakika 180 za timu yake katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kuchelewa usajili wa mashindano hayo alisema mechi hiyo ndiye imebeba mustakabali wao wa msimu ujao na kuthibitisha kikosi cha sasa ni tofauti.

Djuma ambaye ni Mkongomani amesema kuwa baada ya kupoteza mechi zote mbili za CAF na kutupwa nje mchezo muhimu utakaowarudisha katika kuanza kushinda ni dhidi ya Simba ambao unakwenda kuamua safari ya kupata mataji.

Simba itakutana na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambao utakuwa ni ufunguzi wa pazia la ligi katika msimu wa 2021/22 huku Djuma ukiwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano.

“Tumepoteza mechi mbili hakuna ambaye amefurahia hilo binafsi nimeumia sana kwa kuwa naona timu yangu inakosa huduma yangu nikiwa jukwaani lakini soka ndivyo ilivyo,” alisema Djuma ambaye anasifika kwa kupandisha mashambulizi na krosi zenye macho.

“Tumetolewa katika mashindano ya Afrika kitu muhimu sasa ni kurudisha mapambano mapya hapa nyumbani tunatakiwa kusawazisha makosa katika mechi hii inayokuja, tunawaheshimu Simba ni timu kubwa na nzuri lakini uhitaji wetu wa ushindi ndio utaamua mchezo huu,” alisema Djuma ambaye ni raia wa DR Congo akisajiliwa kutokea AS Vita.

KUHUSU CHAMA

Djuma aliongeza alikuwa anaifuatilia Simba ikicheza dhidi ya TP Mazembe na kupoteza bao 1-0, alichogundua bado wana kazi ya kuziba pengo la kiungo Clatous Chama na sasa ubunifu wa eneo la kiungo uko kwa Larry Bwalya.

“Nimeangalia mechi ya Simba walivyocheza na Mazembe walijitahidi kuonyesha uwezo lakini yule Chama (Clatous) bado hawajaweza kupata mtu kama yule alikuwa mbunifu sana,sasa wana Bwalya sioni kama ataweza kutuzuia tusipate ushindi.

“Tunahitaji ushindi huu kuwatuliza mashabiki wetu tumekubaliana na hii itakuwa ni fainali yetu ambayo itatuonyesha safari ya mafanikio,” aliongeza staa huyo anayepambana kurejea kwenye timu yake ya Taifa.


Post a Comment

0 Comments