HANS POPPE KUZIKWA LEO IRINGA,PUMZIKA KWA AMANI


 MWILI wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Zacharia Hans Poppe umeagwa jana mchana na familia yake, nyumbani kwake Ununio, Dar kabla ya kuusafirisha kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi leo Jumatano.

Familia ilipata fursa ya kuuaga mwili wa mpendwa wao nyumbani wakiwemo wachezaji wa Simba B na Simba Queen kabla ya kuanza safari kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya kuupumzisha mwili kwenye makazi ya milele.

Tayari mwili wake umepokelewa Iringa ikiwa na kwa sasa inafanyika ibada ya mwisho kwa ajili ya kuuaga kwa wakazi wa Iringa pamoja na ndugu na jamaa.

Pumzika kwa amani ZHP Post a Comment

0 Comments