NJOMBE WAPIGA HESABU ZA KURUDI LIGI KUU BARA


 UONGOZI wa Chama cha Soka Njombe, (Njorefa) umeweka bayana kuwa wataipambania timu ya Njombe Mji kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara.

Njombe Mji kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Pili iliporomoka msimu uliopita mpaka kutoka Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.

Kwenye dirisha la usajili imesajili jumla ya nyota 28 ikiwa ni pamoja na beki mkongwe James Mwasote ambaye aliwahi kukipiga ndani ya Tanzania Prisons.

Katibu wa Chama cha Soka Njombe, Obedi Mwakasungwa amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri na kuirejesha timu hiyo ndani ya ligi msimu ujao.

"Tumejipanga kufanya vizuri na tumesajili wachezaji wazuri ambao wanatufanya tuamini kwamba baada ya misimu miwili tunarejea kwenye Ligi Kuu Bara.

"Tuna wachezaji wenye uzoefu na imara hivyo ni suala la muda kuona namna gani tunarejea ndani ya ligi,ushirikiano ni jambo la msingi," .

Kwa sasa Njorefa wanaishikilia timu hiyo baada ya kutokuwa na viongozi. Ilipokuwa ikishiriki Ligi Kuu Bara ilikuwa na wachezaji nyota kama Ditram Nchimbi ambaye kwa sasa yupo Yanga pamoja na David Kissu ambaye kwa sasa yupo ndani ya Namungo FC.Post a Comment

0 Comments