Home news YANGA WAKWEPA MITEGO MIWILI NIGERIA…SIMBA YAHUSISHWA

YANGA WAKWEPA MITEGO MIWILI NIGERIA…SIMBA YAHUSISHWA


UAMUZI wa mdhamini wa Yanga, kampuni ya GSM kukodi ndege binafsi ya kuipeleka timu hiyo Nigeria kwa mechi ya marudiano dhidi ya Rivers United, Jumapili ijayo utaisaidia kuruka viunzi viwili ambavyo vingeiweka katika mazingira magumu katika ratiba zilizo mbele yake.

Tathmini iliyofanywa  imebaini kuwa Yanga kama ingetumia usafiri wa ndege za kawaida kama ilivyo kwa abiria wengine kwanza ingekutana na mtego wa ugumu na umbali wa kufika jijini Port Harcourt ambako mchezo huo utachezwa kutokana na mazingira ya nchi ya Nigeria yalivyo.

Ikiwa ingetumia usafiri wa ndege za kawaida ambazo ingelazimika kuunganisha ama kwa kwenda Ethiopia au Kenya, Yanga ingelazimika kutumia siku mbili kwa kwenda hadi Lagos, Nigeria ambako baada ya kutua hapo ingetakiwa tena kusafiri ama kwa basi au kwa ndege hadi Port Harcourt kutakakochezwa mechi hiyo

Kutokana na usafiri wa ndege za kutoka Lagos kwenda Port Harcourt kutokuwa wa uhakika, usafiri wa haraka ambao Yanga ingelazimika kuutumia ni wa basi jambo ambalo ni wazi kwamba lingewachosha wachezaji kutokana na umbali uliopo baina ya mji huo mkuu wa Nigeria na Port Harcourt ambao uko Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Umbali kutoka Port Harcourt hadi Lagos ni Kilomita 627 sawa na umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Manyoni, Singida hivyo kwa usafiri wa basi, Yanga ingelazimika kusafiri kwa muda wa saa 11 na dakika saba.

Kingine Yanga ingetumia ndege za abiria wa kawaida, ingekuwa na uwezekano mkubwa wa kutua hapa Sept. 23, yaani siku mbili tu kabla ya kuivaa Simba kwenye Ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  JEZI YA MTANZANIA YAUZWA UBELGIJI