AZAM FC KUJA NA JAMBO HILI KUBWA


MABOSI wa Azam FC wameamua kuwa karibu na mashabiki wao ambapo siku ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Pramids ya Misri wataweka bonge moja ya screen nje.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza:" Siku zote tunawajali mashabiki wetu, sasa mtaweza kushuhudia mchezo wetu wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri, kwenye luninga kubwa tutakayoifunga nje ya Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 9.00 Alasiri.


"Wakati unashuhudia mbungi hiyo ya viwango, utaweza kupoza koo lako kwa kujipatia viburudisho murua kabisa kutoka Officialbakhersagroup kama vile Maji ya Uhai, Mango Crush, Azam Ice Cream, Azam Ukwaju, Azam Energy, Azam Cola, Juisi za African Fruti, Apple Punch.

"Azam FC tunazidi kuwakumbusha kuwa mchezo huo hautakuwa na mashabiki, watakaoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja tukitekeleza agizo kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF),"Post a Comment

0 Comments