KIBADENI AGUSIA ISHU YA CHAMA NA LUIS,AIONYA SIMBA KUHUSU YANGA

KING Kibadeni amesema kuwa vijana ambao wanacheza mpira kwa sasa wanapaswa kujituma ili waweze kupata ushindi kwenye mechi ambazo wanazipata tofauti na zamani ambapo hakukuwa na wadhamini wao walikuwa wanacheza mpira na kuondoka.

Kuhusu Simba amesema kuwa ina kikosi kizuri ila watu wanapenda matokea na mechi zake za hivi karibuni haikuwa na matokeo mazuri hivyo inapaswa kutokuwa na haraka. Amesema kuwa wale wachezaji wawili ambao waliuzwa ambao ni Luis Miquissone na Clatous Chama ilikuwa ni biashara hivyo pesa iliyopatikana itatumika kutafuta ushindi. 

Amebainisha kuwa ikiwa Simba watazembea Yanga wanaweza kuchukua ubingwa.

 Post a Comment

0 Comments