Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA KUIONA YANGA INAVYOCHEZA..ZAHERA ASHINDWA KUJIZUA..ATOA TAHADHARI KUHUSU SIMBA...


MKURUGENZI wa Maendeleo Soka la Vijana Yanga, Mwinyi Zahera amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba, Yanga ni zaidi ya fainali. “Mechi hizi huwa hazitabiriki lakini ukiangalia Yanga wako imara kwenye kila idara, ingawa hauwezi kuwa mchezo mwepesi kutokana na historia na uhalisia wake,” alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.

Zahera aliongeza kuwa ugumu pia unatokana na mahitaji ya kila timu kutaka kushinda ili kujitengenezea wigo mpana wa pointi ingawa bado ni mapema sana maana michezo yenyewe bado ni michache.

“Ushindi kwa timu yeyote unaweza kutoa taswira ya ubingwa kwa klabu hizi licha ya kuwa ni ngumu kutabiri hivyo kwa kuwa unaweza ukaanza vizuri na ukamaliza vibaya,” alisema.

Zahera alishawahi kuihudumia miamba hiyo ya zamani ya soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC akiwa Kocha mkuu alipojiunga nayo mwaka 2018 na kuiongoza kwenye michezo 63 mpaka kuachana nayo mwaka 2019.

Kwa upande wa kiungo wa zamani wa Simba Henry Joseph ‘Shindika’ alisema; “Unaweza ukaona timu ni dhaifu kuliko nyingine lakini unapoenda kwenye mchezo husika hali hubadilika, hivyo naamini ambaye atajipanga vizuri kisaikolojia ataibuka na ushindi.”

Timu hizo zitakutana Desemba 11, katika uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni mchezo wa kwanza msimu huu wa 2021/22, baina ya miamba hiyo miwili. Simba ilipoteza bao 1-0 kwenye ngao ya hisani.

Reactions

Post a Comment

0 Comments