Home news KUELEKEA SIMBA vs YANGA …MECHI KUISHA KWA SARE? …MWAMUZI ALIYEPANGWA HANA BAHATI...

KUELEKEA SIMBA vs YANGA …MECHI KUISHA KWA SARE? …MWAMUZI ALIYEPANGWA HANA BAHATI NA SIMBA vs YANGA….


Wakati joto la pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya vinara Yanga dhidi ya Simba likizidi kupanda mwamuzi, Herry Sasii amepewa jukumu la kusimama kati kuamua mchezo huo.

Rekodi zinaonyesha kwamba Sasii hii itakuwa mechi yake ya tatu dhidi ya klabu hizo kongwe huku zote mbili zilizopita zikimalizika kwa sare.

Katika orodha ya maafisa watakaosimamia mchezo huo iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania Sasii kutoka Da es Salaam atasaidiwa na kwanza Kassim Mpanga na wa pili akiwa Hamdani Said wote nao kutoka Dar es Salaam huku mwamuzi wa akiba akiwa Ahmada Simba kutoka Kagera.

Mchezo huo utakaoanza majira ya saa 11 jioni Desemba 11 mtathimini wa waamuzi atakuwa Soud Abdi kutoka Arusha wakati mechi kamishna akiwa Hosea Lugano wa Lindi.

ofisa itifaki jukumu amepewa Jacqueline Kamwamu wa Dar es Salaam,Hashim Abdallah akipewa majukumu ya ulinzi.

Ofisa Masoko wa mchezo huo yatakuwa chini ya Fredrick Masolwa huku Afisa Habari akiwa Clifford Ndimbo wote wa Dar es Salaam.

Dawati la matibabu litaongozwa na Dk Norman Sabuni,msimamizi wa kati wa kituo akiwa Msanifu Kondo wote wa Dar es salaam.

Baraka Kizuguto atakuwa Mratibu mkuu wa mchezo akipewa wasaidizi wawili ambao ni Jonathan Kassano na Herieth Gilla wote wakitoka Dar es Salaam.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA