Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

RASMI...YANGA YAFYEKA WANNE..RAMADHAN KABWILI NAYE YUMO...UONGOZI WATOA SABABU HIZI HAPA...

 


KUELEKEA usajili wa dirisha dogo, taarifa zinasema kuwa tayari Kamati ya Usajili ya Yanga imeanza kazi baada ya kuwafyeka wachezaji wanne kwa ajili ya kuwapisha nyota wapya watakaosajiliwa.

Wachezaji wanne wanaotajwa kuachana na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba 15, mwaka huu ni Adeyum Saleh, Ditram Nchimbi, Ramadhan Kabwili na Paul Godfrey ‘Boxer’.

Chanzo chetu kutoka Yanga, kimeliambia gazeti la  Spoti Xtra, kwamba: “Tayari kamati ya usajili imeanza kazi yake kwa ajili ya kuimarisha kikosi wakishirikiana na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

“Kuna wachezaji ambao wataondolewa kwenye kikosi kutokana na kutokuwa na kiwango bora na wengine watatolewa kwa mkopo kuwapisha wachezaji watatu watakaosajiliwa.

“Wachezaji hao ni pamoja na Ditram Nchimbi, Ramadhan Kabwili ambao wote wawili hawapo kambini na wengine ni Adeyum Saleh pamoja na Paul Godfrey.”

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominick Albinus, alisema: “Tumeanza kufanya kazi tayari na tupo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kumalizana na baadhi ya wachezaji ambao tutawaongeza kikosini.

“Hatuna ugumu wowote kwetu kusajili kwani mchezaji yeyote tunayemuhitaji tutamsajili. Wapo wachezaji wawili ambao tunaendelea na mazungumzo nao ili kuwaongezea mikataba.

“Kuhusu suala la wachezaji ambao tutawatoa kwa mkopo bado hatujapewa mapendekezo na kocha ila kuna maeneo yapo kwa ajili ya kuongeza wachezaji, hawawezi kuzidi wawili au watatu.

“Wachezaji ambao tunawasajili kwa sasa hawawezi kuwa wale wa kupewa muda bali tunahitaji wale ambao wataleta faida kwenye timu kwa haraka kwa kuingia kikosini.”

Reactions

Post a Comment

1 Comments

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)