Ticker

6/recent/ticker-posts

random/hot-posts/news

Ad Code

Responsive Advertisement

BAADA YA SIMBA KUWEKEA NGUMU KUMSAJILI..MNIGERIA AVUNJA UKIMYA..AANIKA YALIYOJIRI...

 


KIUNGO Mnigeria, Udoh Etop David, amethibitisha kwamba, hajafanikiwa kupata mkataba wa kuitumikia Simba baada ya kufanya majaribio kwa takribani wiki moja.

Udoh akiwa kwenye majaribio hayo, alifanikiwa kucheza mechi mbili za Kombe la Mapinduzi, lakini ameshindwa kumshawishi Kocha Pablo Franco.

Akizungumza na kunukuliwa na gazeti la  Spoti Xtra, kiungo huyo mkabaji, alisema licha ya kutarajia kupewa makataba na timu hiyo, lakini hajafanikiwa na kwa sasa kitu ambacho anatarajia ni mipango ya safari yake kutoka Tanzania kurudi kwao Nigeria.

“Maisha ya Tanzania ni mazuri na nimeyapenda sana, ndani ya Simba nimekaa vizuri kuanzia kambini hadi kwenye mechi.

“Kuhusu kupewa mkataba na Simba hapana,hakuna maisha mengine tena ndani ya Simba.

“Kwa sasa naangalia mipango yangu ya kuondoka Tanzania kurudi nyumbani Nigeria na leo (jana) Jumamosi naenda kupima vipimo vya Corona, kisha nitaondoka,” alisema mchezaji huyo.

Reactions

Post a Comment

0 Comments