Home news KISA SIMBA KUWAFANYIA MAJARIBIO KINA SHIBOUB..RAGE AIBUKA NA KUTOA POVU HILI..ADAI NI...

KISA SIMBA KUWAFANYIA MAJARIBIO KINA SHIBOUB..RAGE AIBUKA NA KUTOA POVU HILI..ADAI NI NJAA TU….


MABOSI wa Simba mchana wa jana walitarajiwa kumpokea mshambuliaji mwingine nyota wa kigeni kutoka Nigeria, lakini waliopo kambini kwa sasa akiwamo Etoph Udoh, Shiboub Sharifeldin, wameshtua baadhi ya vigogo wa Msimbazi.

Simba imekuwa ikipokea nyota wa kigeni kwa ajili ya kuwafanyia majaribio kabla ya kusajili mmoja kwa nafasi waliyonayo kwa wachezaji wa kigeni na hilo limemfanya Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage aliyeeleza namna alivyoshtushwa na nyota hao.

Rage alisema, kwa namna Simba inavyopokea wachezaji kwa ajili ya majaribio ni wazi nyota hao wa kigeni wamekuja kutokana na kuwa na kusumbuliwa na njaa na hadhani kama watawafaa.

Mbali na Shiboub na Udoh ambaye ni Mnigeria aliyepokelewa juzi, huku kukiwa na taarifa mchana wa jana kuna Mnigeria mwingine, Michael Babatunde anayekipiga Wydad Casablanca ya Morocco inayochezwa pia na nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva.

Simba imeachana na Duncan Nyoni kutoka Malawi aliyesajiliwa msimu huu kabla ya kushindwa kumvutia kocha Pablo Franco aliyeamua kumpiga chini sambamba na wazawa wanne akiwamo Abdulswamad Kassim, Jeremia Kisubi na Ibrahim Ajibu aliyepo Azam FC.

Mchezaji mwingine anayefanyiwa majaribio ni winga Moukoro Cheik kutoka Ivory Coast aliyecheza mechi ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi, kati ya Simba na Selem View akiingia kipindi cha pili kama ilivyokuwa kwa Shiboub aliyewahi kukipiga timu hiyo kabla ya kuachwa.

Pablo ndiye aliyepewa rungu la kuamua nani wa kuziba nafasi iliyowazi kwa nyota wa kigeni kwa ajili ya Ligi Kuu Bara, Kombe la ASFC na Kombe la Shirikisho Afrika Simba ikiwa kundi D.

Akizungumza Hivi karibuni, Rage aliiongoza Simba kati ya mwaka 2010-2014, alisema, wachezaji hao wa kigeni wanaokuja kufanya majaribio dirisha dogo wanachekesha na tafsiri yao kubwa ni njaa ndizo zimewaleta.

“Mchezaji wa kigeni anayejitambua na kujua thamani yake, hawezi kuja kufanyiwa majaribio katika dirisha dogo, hata siku moja duniani kote haipo hiyo,” alisema Rage na kuongeza;

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA KUDAIWA KUWA TAYARI WAMESHAMNASA....MPOLE AIBUKA NA HILI JIPYA....ADAI HUU NI MUDA WA MAVUNO...

“Mchezaji wa Kigeni anatakiwa kuja na kuingia moja kwa moja kwenye timu acheze na sio kuanza kupimwa, hayo mambo ya majaribio ni dirisha kubwa. Katika dirisha dogo unachukua mtu unayemjua na kumfahamu vilivyo kwa lengo la kukusaidia sehemu iliyopwaya.”

Rage alisema pia, kwa namna uongozi wa Simba unaofanya sasa ni matumizi mabaya ya pesa kwa kuwa haoni mantiki ya wachezaji wote hao kuja Tanzania wakati wanahitaji mmoja pekee.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji alipoulizwa juzi juu ya ujio wa wachezaji hao alisema hawaoni tatizo, ila maamuzi ya mwisho ni ya kocha wao kuamua nani wamsajili kama atawafaa na ikishindikana wataaga nao kiroho safi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here