Ticker

6/recent/ticker-posts

KISA USAJILI WA CHAMA..MANARA ATUPA DONGO SIMBA...AMTAJA HERSI...


Msemaji wa Yanga Haji Manara amerusha kombora kwa watani wao  akisema akisema vinara hao wa ligi hawasajili wachezaji kwa kificho.

Manara ameyasema hayo jana akisema bila kuitaja jina Simba akidai usajili unaofanywa na mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga Hersi Said ni mambo ya wazi ya kujiamini.

Manara lisema zipo klabu zimekuwa zikiwaficha wachezaji kwa barakoa na nguo nyingi huku wakitaka mashabiki wao kubashiri njia ambazo Yanga hazizitumii

"Huyu Hersi ni mtu balaa sana anafanya mambo yake kwa uwazi akishusha mtu anaweka wazi hakuna kufichaficha mara mchezaji mnamvalisha barakoa hakuna hiyo tunakwenda mambo moja kwa moja,"amesema Manara

"Zipo klabu zimekuwa zikiwavalisha manguo makubwa wachezaji lakini huku hakuna hiyo mtu analetwa na mambo yanakuwa wazi.

"Sasa hivi Hersi amekuwa na mtindo wake flani hivi anakaa anachambua kwa video pale na anatuonyesha sio kule kwingine mambo sirisiri yaani chupli chupli tu."

Reactions

Post a Comment

0 Comments