Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

MKE AINGILIA KATI SAKATA LA FRAGA KURUDI SIMBA...ATOA MASHARTI MAZITO KWA UONGOZI...


Imefahamika kuwa mke wa kiungo wa kutoka nchini Brazil Gerson Fraga amemzuai mume wake kuja Tanzania kufanya majaribio, baada ya kupokea wito kutoka kwa Mabingwa wa Soka Simba SC.

Fraga alitajwa huenda angejiunga na kikosi cha Simba SC kisiwani Unguja-Zanzibar kwa kufanya majaribio kabla ya kurejeshwa jumla kikosini.

Taarifa zinaeleza kuwa mke wa kiungo huyo aliyejizolea umaarufu kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kufuatia kucheza jihadi eneo la kiungo wa kati, amemzuia mumewe kwa kuamini hapaswi kufanyiwa majaribio.

Mke wa Fraga anaamini Viongozi wa Simba SC walipaswa kumsajili moja kwa moja mume wake kutokana na kuwahi kuitumikia klabu hiyo kabla ya kusitishiwa mkataba wake msimu uliopita.

Fraga aliondoka Simba SC baada ya kupata jeraha la goti kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC na nafasi yake ilijazwa na Kiungo Thadeo Lwanga.

Kuumia kwa kiungo huyo kutoka nchini Uganda ndio kumeibua mpango wa kurejeshwa kwa Fraga, lakini mpango huo unaonekana kukwama.

Reactions

Post a Comment

0 Comments