Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

ILE ISHU YA CHAMA KURUDISHWA DAR WAKATI WENZAKE WAKIJIANDAA NA YANGA MWANZA KUMBE CHANZO NI HIKI...


Kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Simba Clatous Chama hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Yanga Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza baada ya jana kuondoka kambini.

Inaelezwa Chama alienda Mwanza lakini hakuwa fiti baada ya kupata majeraha siku kadhaa zilizopita huku akiruhusiwa kurejea Dar es Salaam jana.

Baada ya Simba kutua Mwanza Chama alianza mazoezi na wenzake lakini juzi alipelekwa hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi na kubaini anahitajika matibabu zaidi.

Mbali na kurejea Dar es Salaam nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda nchini kwao Zambia kushiriki mwaka mmoja wa kifo cha marehemu mke wake aliyefariki dunia Mei 28 mwaka jana.

Reactions

Post a Comment

0 Comments