Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

KUHUSU ISHU YA KUTEMANA NA YANGA...NTIBAZONKIZA APANGA KUTAPIKA NYONGO..."SITARUHUSU MTU ANICHAFUE"...


Ikiwa ni muda mfupi baada ya kuibuka taarifa kumuhusu kiungo Saido Ntibazonkiza raia wa Burundi kudaiwa kuachana na Yanga sc, Saido mwenyewe ameibuka na kukanusha taarifa hizo.

"Uongo hutembea kwa kasi, ukweli huchelewa kufika, kamwe sitoruhusu mtu yeyote kuchafua jina langu, baada ya mechi nitaongea. Najua umuhimu wa mechi ya Jumamosi, kwa nguvu za Allah tutapata ushindi. Naipenda sana Yanga," Saido Ntibazonkiza.

Taarifa zilizokuwa zinasambaa zikidaiwa ku kutoka ndani ya klabu ya Yanga, zinasema klabu hiyo imefikia uamuzi wa kuachana na nyota wake, Saido Ntibazonkiza kufuatia makosa ya kinidhamu ya hivi karibuni na kile kimachodaiwa kuwa Saido aligomea kusaini mkataba mpya kuendelea kusalia klabuni hapo.

Reactions

Post a Comment

0 Comments