Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

A-Z JINSI FEI TOTO ALIPODHIHIRISHA THAMANI YAKE YA BILIONI MOJA JANA...CHIKO USHINDI AMTIMULIA VUMBI MAYELE...


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022, Timu ya Yanga wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kufanikiwa kuichapa Polisi Tanzania magoli 2-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Magoli ya Yanga katika mchezo wa jana yamefungwa na Feisal Salum 12' na winga Chico Ushindi 18' kipindi cha Kwanza.

Huu ulikuwa ni mchezo wa 28 kwa Yanga msimu huu na bado wanaendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo msimu huu huku wakiwa wamebakiza michezo miwili kumaliza msimu.

Wakati Yanga wakitakata na ushindi huo nyumbani, Mshambuliaji wake na kinara wa mabao kunako Ligi Kuu hakufanikiwa kupachika bao katika mchezo huo.

Kwa ushindi huo Yanga wanafikisha alama 70 baada ya michezo 28, na Polisi Tanzania wakibaki na alama zao 36 katika nafasi ya 7

Reactions

Post a Comment

0 Comments