Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

GOLI LA FEI TOTO JANA LAONGEZA BILIONI MBILI YANGA...MANARA ATAMBA KILA KONA ...AMFANANISHA NA JEMSHID....


Baada ya siku ya jana asubuhi Juni 22, Msemaji wa Yanga, Haji Manara kutangaza kuwa Kiungo nyota wa Timu hiyo Feisal Salum "Fei toto" hauzwi bila dau la Bilioni 3.

Sasa leo Juni 23, 2022 bei ya Kiungo huyo imepanda maradufu na kwa yeyote atakaevutiwa na huduma yake inabidi ajipange.

Kilichomfanya Fei toto bei yake kupanda ni bao alilowatungua Polisi Tanzania usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara katika dimba la Benjamin Mkapa.

Sasa Msemaji wa Yanga Haji Manara, leo kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika:

Tumepandisha Dau,.

Bila Bilioni Mbili, He Is Not For SALE.

Chini ya hapo, wahi kununua Zabibu Kwa @anthonymavunde kule Dodoma, Au kimbilia Mtwara, Ufuta ndio kipindi chake hiki.

Fesal ni zaidi ya Magician, Yy ndio SULTANI wa Zanzibar baada ya kuondoka kina Jemshid na wenzie, Wao walitawala Nchi,,Mwanamme anatawala Uwanjani.

Reactions

Post a Comment

0 Comments