Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

WAKATI YANGA WAKIWA KWENYE NAFASI YA KUMPATA MPOLE...SIMBA WAPANGA KUPINDUA MEZA KIBABE ...'WAANZA FUJO'....


UMAFIA! Ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya mabosi wa Simba kumfuata mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole na kumtangazia ofa nono ili asaini Msimbazi.

Inaelezwa kuwa Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kuonyesha nia ya kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo ambaye anachuana katika kuwania ufungaji bora na Mkongomani, Fiston Mayele wote wenye mabao 14.

Mpole ni kati ya washambuliaji wazawa walioonyesha kiwango bora katika msimu huu ambaye juzi aliifungia Stars bao la kuongoza katika kuwania kufuzu Afcon walivyocheza dhidi ya Niger ugenini mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mpole amekuwa na msimu mzuri akiwa na jumla ya mabao 14 hadi sasa

Taarifa zinasema kuwa Simba imemfuata kimyakimya mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kuipata saini ya staa huyo wa Geita inayofundishwa na mzawa Fred Minziro.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mshambuliaji huyo bado hajachukua maamuzi wapi atakwenda kati ya timu hizo mbili katika msimu ujao.

Aliongeza kuwa mazungumzo yanakwenda vizuri kati ya mshambuliaji huyo na timu hizo mbili kubwa hapa nchini zenye ushawishi wa usajili ambazo wachezaji wengi wanatamani kuzichezea.

“Tunafahamu tuna ushindani mkubwa katika usajili wa wachezaji wa ndani na nje ya nchi, lakini kama sisi Simba hatufanyi papara zaidi tutajipanga vema kuhakikisha tunafanikisha mahitaji ya wachezaji tutakaowahitaji.

“Mpole tupo katika mazungumzo mazuri kwa ajili ya kumsajili kama mipango ya usajili ikienda vizuri, kwani ni kati ya washambuliaji wazawa waliokuwepo katika kiwango bora msimu huu.

“Kama mipango itakwenda sawa, basi tutafanikisha usajili wa Mpole kwa ajili ya msimu uajo katika kuiboresha safu yetu ya ushambuliaji,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema kuwa: “Usajili wetu utafanywa na kocha wetu mpya atakayekuja kuifundisha katika msimu ujao.

“Usajili wetu hautakuwa na kelele nyingi kama ilivyokuwa kwa hao wenzetu, sisi usajili ukikamilika haraka tutauweka wazi.”

Reactions

Post a Comment

0 Comments