Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA SIKU KADHAA KUPITA TOKA ATAMBULISHWE YANGA...MORRISON AKUMBUSHIA JINSI ALIVYOONDOKA NA KUTUA SIMBA...


Kiungo wa kimataifa wa Ghana aliyejiunga na Yanga SC kama mchezaji huru akitokea Simba SC Benard Morrison ameandika ujumbe mzito kwa mashabiki wa Yanga ambao waliumia na kuondoka kwake na kujiunga na Simba SC sasa anasema amerudi nyumbani.

“Nilikuwa hapa nikaondoka sasa nimerudi tena naamini ujio huu wa pili utakuwa mkubwa kuliko ule wa mara ya kwanza nilipendwa na taifa hili la rangi ya njano na kijani na bado mnanipenda”

“Najua nilisababisha maumivu na aibu bado mmenikubali mtoto wenu nirudi nyumbani, sababu sote tunajua msemo wa nyumbani kutamu kijana wenu nimerudi na nitafanya niwezavyo kuwafanya muwe na furaha kila mahali na wakati wote”

“Tushirikiane kuiweka club hii kubwa kwenye jukwaa la kimataifa kama ilivyokuwa ikifanya hapo awali”

Reactions

Post a Comment

0 Comments