Ticker

6/recent/ticker-posts

HILI HAPA JESHI LA STARS DHIDI YA SOMALIA...MASTAA WA SIMBA NA YANGA KAMA KAWA WATAWALA...


Kocha mkuu wa Taifa Stars,  Mdenmark Kim Poulsen ametangaza kikosi kitakachoingia kambini Julai 15, 2022, kujiandaa na  Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani  (CHAN).

Stars itacheza mechi mbili dhidi ya Somalia, hivyo wachezaji watatakiwa kuingia kambini Ijumaa kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni katika hotel ya Diamond Tiffany.

Wachezaji waliyoitwa kwenye kikosi hicho ni Aishi Manula, Metacha Mnata, Abwatwarib Mshery, Kibwana Shomari, Lusajo Mwaikenda, David Luhende, Pascal Msindo, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Nickson Kibabage.

Wengine ni  Mzamiru Yassin, Aziz Andambwile, Kelvin Nashon, Mudathir Yahaya, Feisal Salum 'Fei Toto' Farid Mussa, Abdul Suleiman 'Sopu', Reliants Lusajo, Kibu Denis, George Mpole, Anwari Jabir, Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Reactions

Post a Comment

0 Comments