Home Habari za michezo KISA MASTAA WA KIMATAIFA WANAOSAJILIWA MSIMBAZI… BEKI KISIKI AZUIWA KUSAINI SIMBA…FAMILIA...

KISA MASTAA WA KIMATAIFA WANAOSAJILIWA MSIMBAZI… BEKI KISIKI AZUIWA KUSAINI SIMBA…FAMILIA YAINGILIA KATI..


Beki mpya wa Singida Big Stars ‘SBS’ Abdulmajid Mangalo ameelezea jinsi ambavyo familia na wasimamizi wake walivyomkataza kujiunga Simba.

Mangalo amejiunga SBS kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Biashara United ya mkoani Mara ambako alihudumu misimu minne huku akiwa Nahodha wa timu hiyo.

Akizungumza Mangalo alisema alikubali kujiunga Simba kutokana na kumsumbua kwa muda mrefu lakini baadhi ya washauri walimkataza.

“Binafsi nilikuwa tayari kucheza Simba lakini kuna ushauri lazima niupokee kwa sababu sipo peke yangu, nyuma yangu kuna watu zaidi kama watatu au wanne na familia wanakuwa watano.

“Kwa hiyo siwezi kufanya maamuzi ya moja kwa moja bila ushauri wa ndugu zangu wananishauri na mwenyewe huchanganua hivyo niliona ni sahihi,” alisema na kuongeza;.

“Kwa sababu zile timu ukiangalia bado zina presha kubwa, zinataka kutengeneza timu na zinataka matokeo lazima presha iwe kubwa, hivyo ofa ya Simba ilipokuja nilishirikisha familia yangu ambayo ilinishauri nicheze kwanza huku chini hata miaka miwili nitakuwa nimekomaa na presha ya timu hizo,” alisema

Beki huyo alisema licha ya wingi wa mastaa wanaoendelea kusajiliwa na kikosi hicho ila wasitarajie mteremko bali wanapaswa kupambana kwa ajili ya kuleta ushindani.

“Wengi wanataka kuona tutafanya nini msimu ujao, sio mashabiki wetu na viongozi tu bali hata watu walioko nje hivyo tuna deni kubwa sana kwao,” alisema Mangalo

Naye Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Muhibu Kanu alisema jambo watakalolifanya kwa nyota wao ni kuhakikisha kila kitu wanakipata kwa wakati kuanzia maslahi binafsi kwa sababu malengo yao makubwa ni kuleta ushindani msimu ujao.

Mbali na Mangalo aliyesajiliwa ila wapo nyota wengine waliotambulishwa ambao ni kiungo, Aziz Andambwile (Mbeya City), Paul Godfrey ‘Boxer’ (Yanga) na Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar).

SOMA NA HII  GOMES: NINAIJENGA SIMBA YA MISIMU MINNE IJAYO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here