Ticker

6/recent/ticker-posts

SAA CHACHE BAADA YA KUTANGAZWA KUWA AMECHWA...KASEKE AJIBU MAPIGO.. AIBUKA NA WARAKA HUU KWA YANGA...


Klabu ya Yanga SC, leo Alhamisi, Julai 14, 2022 imetangaza kuachana na mchezaji wake mwandamizi, Deus Kaseke ‘Mwaisa’ (27) na kumtakia kila kheri aendako ambapo.

Katika taarifa fupi ya Yanga isiyozidi maneno 20 imesema; "Umekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio kwenye Klabu yetu, tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako."

Kwa upande wake, Kaseke kupitia ukurasa wake wa Instagram ameishukuru Yanga kwa kipindi chote ambachpo ameitumikia.

"Asante sana Yanga mmekuwa sehemu kubwa saana ya maisha yangu ya mpira, nashukuru kwa sapoti kubwa mlionipa kipindi chote nilichotumikia Timu ya Wananchi, asanteni sana Wananchi.

Kaseke ameitumikia klabu hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka mitano akishinda mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Tetesi zinasema Mnyakyusa huyo anawindwa na walima alizeti Singida Big Stars.

Mbali na Yanga, Kaseke pia amewahi kuzitumikia timu za Singida United na Mbeya City ya nyumbani kwao kwa nyakati tofauti.

Reactions

Post a Comment

0 Comments