Home Habari za michezo SAA CHACHE TOKA MORRISON ATANGAZWE KUTUA YANGA…MAYELE AIBUKA NA DONGO HILI LA...

SAA CHACHE TOKA MORRISON ATANGAZWE KUTUA YANGA…MAYELE AIBUKA NA DONGO HILI LA KUMKARIBISHA…


Straika wa Klabu ya Yanga ambaye ni raia wa Congo DR, Fiston Kalala Mayele amemkaribisha aliyekuwa staa wa Simba Sc, Bernard Morrison katika familia ya Yanga ili kuitumikia klabu hiyo.

Mayele kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameposti picha ya Mayele na kuandika maneno haya “Name the Player in EPL terms?” akimaanisha “Mtaje mchezaji huyu kwa vigezo vya EPL (Ligi Kuu ya Uingereza)?”

Usiku wa kuamkia leo, Klabu ya Yanga imemtangaza Morrison ambaye ni raia wa Ghana kuwa mchezaji wake akitokea kwa mahasimu wao wa jadi, Simba Sc ambako amemaliza mkataba wake.

Ikumbukwe kuwa, Morrison amewahi kucheza Yanga, nusu msimu wa mwaka 2019/2020 kabla ya kutimkia Simba ambako ameitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili na kisha sasa anarejea tena Yanga.

Hivi karibuni kumekuwepo na stories nyingi kuhusu Morrsion kushindwana na Simba huku yeye akifunguka kuwa katika mkataba wake mpya walimpunguzia mshahara jambo ambalo hakukubaliana nalo hivyo ameamua kuondoka.

SOMA NA HII  YANGA BADO TATU TU....