Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA KUZUNGUKA KOOTEE HUKO....HATIMAYE JAMES KOTEI NJIANI KURUDI SIMBA...AJIUNGA NA MTIBWA KUJIWEKA KARIVU ZAIDI..


KIUNGO wa Singida Big Stars, James Kotei amekamilisha kujiunga Mtibwa Sugar kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Akizungumza Kotei alisema hakuna tatizo juu ya uhamisho huo kwani viongozi wa Mtibwa wameonyesha nia ya dhati ya kumhitaji kufanya nao kazi licha ya kuanza maandalizi na waajiri wake.

“Ni uamuzi binafsi na sio shinikizo lolote. Nipo tayari kutoa mchango wangu kuiwezesha timu kufanya vizuri kwani hilo linawezekana kutokana na ushirikiano baina yetu wachezaji, benchi la ufundi na viongozi,” alisema

Kocha wa kikosi hicho, Salum Mayanga alisema mambo yanayomvutia ni ubora wa nyota wapya waliosajiliwa huku akiamini wataleta ushindani kwenye mashindano mbalimbali tofauti na msimu uliopita.

Kotei ambaye aliwahi kuichezea Simba licha ya kujiunga na Mtibwa, hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili na Singida akiungana na nyota wengine wapya.

Reactions

Post a Comment

0 Comments