Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMA ULIKUWA HUJUI....HUYU HAPA NDIO TEPSIE ANAYEMPA NABI MAWAZO ...KAANZA KUSUMBUA WATU MAPEMA SANA...


Kuelekea mechi ya ligi kuu na Yanga, Nyota wa Azam FC, Tepsi Evance ni miongoni mwa wachezaji walioanza ligi wakiwa kwenye ubora akihusika na mabao matatu ya timu hiyo iliyofunga katika mechi mbili za kwanza huku mwenyewe akisema “huo ni mwanzo tu”.

Tepsi alianza kuonyesha ubora kwenye mechi ya kwanza ya ligi msimu huu dhidi ya Kagera Sugar akitoa asisti kwa Prince Dube aliyeisawazishia Azam na kufunga bao la pili la ushindi mbele ya Kagera Sugar mchezo ukimalizika kwa matajiri hao wa Chamazi kushinda mabao 2-1.

Nyota huyo aliyetokea akademia ya Azam hakuishia hapo kwani katika mchezo wa pili dhidi ya Geita Gold uliomalizika kwa sare ya 1-1 ndiye aliyepachika bao pekee la Azam huku akionyesha kiwango bora zaidi.

Akizungumzia ubora wake, Tepsi ameeleza kuwa huo ni mwanzo tu na amejipanga kufanya zaidi kila atakapopewa nafasi.

“Kila mchezaji anatamani kufanya vizuri na kuisaidia timu yake kupata matokeo chanya. Nafurahi kwa kufanya vizuri katika mechi mbili za mwanzo na natarajia kufanya vizuri zaidi,” alisema Tepsi.

“Mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono na naamini nitaendelea kufanya makubwa kila nikipata nafasi ya kufanya hivyo.”

Mchambuzi wa soka, Salama Ngale alimuelezea Tepsi kama mchezaji mwenye kiu ya mafanikio na siku za karibuni amekuwa kwenye kiwango bora.


Reactions

Post a Comment

0 Comments