Ticker

6/recent/ticker-posts

KUELEKEA SIKU YA WANANCHI...YANGA HAWATAKI DENI AISEEE...WAALIZANA KIMYA KIMYA NA MAYELE...DILI LA SAUZI LAFAA..


Taarifa za ndani kabisa kutoka Klabu ya Yanga zinasema kuwa, mshambuliaji wao kinara raia wa Congo Dr, Fiston Kalala Mayele ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kusalia kunako mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

Mayele ambaye alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2021/2022 alikuwa amesalia na mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia Wananchi, lakini kwa kuongeza mkataba huo mpya, sasa atakuwa na miaka miwili zaidi Jangwani hadi mwaka 2024, ambapo sasa anasubiri kutangazwa tu.

Ikumbukwe kuwa kinara huyo wa mabao kwa Yanga msimu uliopita alikuwa akiwindwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Al Hilal ya Sudan lakini mabosi wa Yanga walisema hauzwi kwani wana mpango naye.

Mbali na Mayele, Yanga pia imemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake mkuu, Nasredine Mohammed Nabi 'Profesa' ambaye ataendelea kukinoa kikosi hicho hadi mwaka 2024 na tayari ameshatangazwa.

Malengo ya Yanga msimu mpya ujao ni kuendelea kutetea mataji yote waliyonyakua msimu uliopita pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Msimu uliopita Yanga waliondoshwa katika hatua ya awali ya mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, hivyo mwaka huu hawataki kurudia makosa yaleyale, ndiyo sababu kuu ya kufanya usajili mkubwa wa Kimataifa wakiwemo Aziz Ki, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana, Lazarous Kambole na Bernard Mossrion.

Reactions

Post a Comment

0 Comments