Ticker

6/recent/ticker-posts

SAA CHACHE BAADA YA YANGA 'KUMPANGUSA KAZI'...BUMBULI AIBUKA NA UJUMBE HUU...ATAJA ANAPOENDA KUFANYA KAZI...


Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli ametangaza rasmi kumalizana na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani.

Kupitia ujumbe wake kwa wanahabari Bumbuli amewashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chake chote.

“Ndugu zangu, naomba kutumia fursa hii, kuwashukuru kwa ushirikiano wenu katika kipindi chote nilichokuwa Afisa Habari wa Klabu ya Yanga.”

“Nawaaarifu rasmi kwamba nimemaliza mkataba wangu wa kuitumikia timu ya Yanga na sasa narejea kwenye majukumu yangu mengine.”

“Nawashukuru sana kwa Umoja wenu, ushirikiano wenu katika kipindi chote tulipokuwa pamoja.”

Mpaka sasa Mrithi wa Hassan Bumbuli katika kitengo cha Afisa Habari ndani ya Yanga hajatangazwa.

Reactions

Post a Comment

0 Comments