Ticker

6/recent/ticker-posts

ZA NDAANI KABISA...WAKATI MASHABIKI WAKIMSUBIRI KWA HAMU....DILI LA MANZOKI KUTUA SIMBA LAOTA MBAWA...UKWELI HUU HAPA...


Mshambuliaji wa Vipers FC ya Uganda, Cesar Manzoki, muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa na moja ya klabu ya nchini China, kisha baada ya hapo atajiunga na Simba baada ya miezi mitatu kupita.

Nyota huyo alikuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Simba kipindi hiki cha usajili ambao utafungwa Agosti 31, mwaka huu kabla ya Yanga kuingilia kati kuwania saini yake.

Manzoki mwenyewe alikuwa tayari kujiunga na Simba mara baada ya kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili kukipiga Msimbazi.

Mmoja wa mabosi wa Simba, amelisema, mshambuliaji huyo atajiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea China ambapo anaenda kucheza kwa sasa.

Bosi huyo alisema klabu hiyo ya China ambayo kwa sasa imefichwa jina lake, imekubali kutoa dau la usajili ambalo Vipers wamelitaka ili kumalizia muda wa mkataba wake uliosalia kikosini hapo, kisha atajiunga na Simba.

Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo amekubali kutimkia China ambako atacheza kwa miezi mitatu, baada ya kumaliza mkataba wake, atajiunga na Simba kipindi cha dirisha dogo ambapo muda huo atakuwa ameimarika zaidi kiuchezaji, hivyo atakuwa msaada kikosini kwao.

“Tumeona ugumu mkubwa juu ya usajili wa Manzoki na klabu yake ya Vipers ambapo inatuchanganya juu ukomo wa mkataba wake.

“Yeye mwenyewe mchezaji ameweka wazi amebakisha miezi mitatu ambayo ataitumia kwenda kucheza soka China na atajiunga na kambi ya Simba mara baada ya ukomo wa mkataba wake huo.

“Hivyo rasmi atakuwepo katika mipango ya timu katika dirisha dogo baada ya kumalizana na klabu hiyo ya China ambayo yenyewe imekubali kutoa dau ambalo Vipers wanalitaka,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Bado usajili wa Manzoki haujakamilika kutokana na klabu yake ya Vipers kuweka ugumu.”

Reactions

Post a Comment

0 Comments