Ticker

6/recent/ticker-posts

RASMI...BAADA YA KUSHINDA MECHI TATU ....SIMBA WAAMUA KUTULIA MAZIMA NA MGUNDA....ISHU YA KOCHA MPYA BADO...


Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema unaridhishwa na utendaji wa kocha Juma Mgunda na msaidizi wake Seleman Matola.

Mwenyekiti wa timu hiyo Murtaza Mangungu amesema mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea lakini kwa sasa walimu waliopo wanaitendea klabu hiyo.

“Mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea vizuri lakini kwa kasi ndogo sana hii inatokana kazi nzuri anayofanya kocha Mgunda na msaidizi wake,” amesema Mangungu.

Amesema kwa kiasi kikubwa wachezaji wamemwelewa Mgunda na hiyo ni kutokana na kiwango wanachokionesha. Mgunda amechukua mikoba ya Zoran Maki aliyefutwa kazi wiki tatu zilizopita.

Reactions

Post a Comment

0 Comments